Mhe. Balozi Dkt. Elsie Sia Kanza alikutana kwa mazungumzo na Maj. Gen. Craig W. Strong, Mkuu (Adjujant General) wa Kikosi cha Walinzi wa Taifa cha Nebraska (National Guard) aliyeambatana na maafisa wengine wa Kikosi hicho Ubalozini Washington, D.C. Kikao hicho kilijadili namna ya kuimarisha ushirikiano baina ya Tanzania na Kikosi hicho na jimbo la Nebraska kwa ujumla wake, katika maeneo mbalimbali muhimu. 

Itakumbukwa kuwa Machi 2026, Tanzania kupitia Jeshi la Wananchi la Tanzania (JWTZ) ilisaini  Makubaliano ya Ushirikiano na Kikosi tajwa kuanzisha Programu ya Ushirikiano wa Majimbo.