Mhe. Balozi Dkt. Elsie Sia Kanza alikuwa mgeni rasmi kwenye hafla iliyoandaliwa na taasisi iitwayo UBORA ya Atlanta, Georgia, kwa ajili ya kuchangisha fedha kwa ajili ya miradi mbalimbali ya kijamii ambayo taasisi hiyo inaifadhili nchini Tanzania. Hafla tajwa ilihudhuriwa na washiriki takriban 250 wakiwemo wafanyabiashara, Viongozi wa serikali ya jimbo la Georgia, viongozi wa dini, wahisani, na diaspora wa Tanzania wanaoishi jimboni humo. 

UBORA ni taasisi isiyo ya kiserikali na ya kidini inayofanya kazi nchini Tanzania kwa lengo la kuleta mabadiliko ya kijamii kupitia elimu na uongozi.

Kwenye hotuba yake, pamoja na masuala mengine, Mhe. Balozi alieleza uwekezaji mkubwa uliofanywa na serikali kwenye sekta mbalimbali za kijamii ikiwemo elimu na kuishukuru taasisi hiyo kwa kuchangia kwenye maendeleo hayo. Aidha, Mhe. Balozi aliahidi ushirikiano zaidi kutoka kwa Serikali.

Aidha, pembezoni mwa halfa hiyo, Mhe. Balozi alikutana kwa mazungumzo na Meya John Bradberry wa jiji la Johns Creek, viongozi wengine wa jiji hilo pamoja na viongozi wa chemba ya biashara ya jiji tajwa ambao alijadiliana nao kuhusu fursa za biashara na uwekezaji nchini Tanzania, na kuwakaribisha kuwekeza.