Mhe. Balozi Dkt. Elsie Sia Kanza, amekutana kwa mazungumzo na Dr. Faruk Taban, Rais wa North American University kilichopo Houston, Texas, kuhusu fursa mbalimbali za ushirikiano baina ya Chuo hicho na Tanzania. Mazungumzo hayo yamefanyika jijini Dallas, Texas, pembezoni mwa Mkutano Mkuu wa Biashara wa Marekani na Africa (US-Africa Business Summit)

Katika mazungumzo hayo, Rais huyo wa North American University ameonesha utayari wa kushirikiana na vyuo vikuu vya Tanzania na kutoa ufadhili wa masomo kwa Watanzania wenye sifa ya kujiunga na Chuo hicho.