Ubalozi umeadhimisha Siku ya Muungano (National Day) kwa kufanya mkutano wa kibiashara (business luncheon) uliohusisha wadau mbalimbali jijini Washington, D.C. Mkutano huo ulijadili namna nchi inavyotekeleza diplomasia ya uchumi ambapo kampuni mbalimbali zilizowekeza Tanzania zilizungumza kueleza uzoefu wao chanya wa kufanya biashara nchini Tanzania, na hivyo kuhamasisha kampuni nyingine kufanya biashara Tanzania.
Maadhimisho hayo yalihudhuriwa na Balozi Eric Kneedler, Kiongozi Mwandamizi kutoka Ofisi ya Masuala ya Afrika, Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani, Viongozi wa jiji la Washington, D.C., Jumuiya ya kidiplomasia, Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa, kampuni za biashara, wanadiaspora wa Tanzania, taasisi za tafiti (think tanks) na marafiki wengine wa Tanzania.
Kwenye hotuba zao, pamoja na masuala mengine, Mhe. Balozi Dkt. Elsie Sia Kanza na Balozi Kneedler walisisitiza umuhimu wa kuimarisha uhusiano wa kihistoria baina ya Tanzania na Marekani ukiwemo uhusiano wa kiuchumi.



