Mwezi Januari 2025, Mhe. Balozi Dkt. Elsie Sia Kanza alifanya mkutano kwa njia ya mtandao na diaspora wa Tanzania nchini Marekani. Kwenye mkutano huo, pamoja na mambo mengine, Mhe. Balozi aliwashukuru diaspora kwa ushirikiano wao kwa mwaka 2024, aliwaomba ushirikiano zaidi mwaka 2025; pia aliwatakia heri nyingi kwa mwaka 2025. Vilevile, Mhe. Balozi na diaspora walibadilishana mawazo kuhusu masuala mbalimbali muhimu yanayohusu maendeleo ya Tanzania na ustawi wa diaspora.