Mhe. Balozi Dkt. Elsie Sia Kanza alikuwa mgeni mwalikwa wa Shule ya Masuala ya Kimataifa ya Chuo Kikuu cha Yale (Yale Jackson School of Global Affairs) ambapo alitoa mhadhara hapo kuhusu mchango wa Tanzania kwenye masuala ya kisiasa na uchumi barani Afrika. Mhadhara huo pia ulihusisha  mkakati wa Ubalozi katika utekelezaji  wa diplomasia ya uchumi nchini Marekani na Mexico pamoja na kuainisha baadhi ya mafanikio yaliyopatikana.
Aidha, Mhe. Balozi alikutana kwa mazungumzo na Uongozi wa Shule hiyo (Dean and Associate Dean) kuhusu kuanzisha uhusiano baina na Tanzania na Shule hiyo ambapo uongozi huo ulionesha utayari wa kufadhili masomo kwa Watanzania wenye sifa za kujiunga na shule hiyo. Ubalozi unafuatilia fursa hiyo.