Mhe. Balozi Dkt. Elsie Sia Kanza akiwa pamoja na Mabalozi wengine wa nchi za Afrika hapa Marekani wanaonufaika na Mfuko wa Maendeleo ya Kimataifa (IDA) wa Benki ya Dunia katika mkutano baina ya Mabalozi hao na Wakurugenzi wa Benki hiyo. Mkutano huo ulijikita katika kujadili mikakati ya Benki hiyo ya kuongeza makusanyo ya fedha za kufadhili miradi ya maendeleo kupitia mpango wa IDA21 ambao utaanza kutekelezwa mwaka 2025. Tanzania ni miongoni mwa nchi zinazonufaika zaidi na fedha za masharti nafuu zinazotolewa na IDA katika nchi zinazoendelea.