Mhe. Balozi Dkt. Elsie Sia Kanza alipata heshima ya kuwa mgeni mzungumzaji kwenye hafla ya ufunguzi wa kituo cha huduma kwa jamii kilichojengwa kumuenzi Jaji Thurgood Marshall (The Justice Thurgood Marshall Amenity Center) jijini Baltmore, Maryland. Jaji Marshall alikuwa ni Mwanasheria wa haki za kiraia ambaye aliteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Marekani, uteuzi uliomfanya kuwa Jaji wa Kwanza Mmarekani mwenye asili ya Afrika kushika wadhifa huo. Jaji Marshall anakumbukwa pia kwa urafiki wake na nchi za Afrika ikiwemo mchango wake katika kuandaa rasimu za sheria na katiba za baadhi ya nchi za Afrika kwenye miaka ya 1960.