Mhe. Balozi Dkt. Elsie Sia Kanza amekutana kwa mazungumzo na Mhe. Thomas Bruns, Waziri Mdogo (Deputy Assistant Secretary) wa Wizara ya Biashara ya Marekani, anayeshughulikia Mashariki ya Kati na Afrika. Mazungumzo yao yalijikita katika kuimarisha uhusiano baina ya Tanzania na Marekani kwenye maeneo ya biashara na uwekezaji ikiwemo mikakati ya kuchochea matumizi ya TEHAMA katika kufungua fursa za kiuchumi kwa wananchi.