Mhe. Balozi Dkt. Elsie Sia Kanza ameongoza uzinduzi wa Chemba ya Biashara ya Tanzania na Marekani (Tanzanian American Chamber of Commerce) ambapo pia alikuwa Mgeni Rasmi. Uzinduzi huo umefanyika jijini Dallas, Texas pembezoni mwa Mkutano Mkuu wa Biashara wa Marekani na Afrika (U.S.- Africa Business Summit). Chemba hiyo ya Biashara ndiyo imepewa jukumu la kuendesha Ofisi ya Tanzania ya Biashara iliyozinduliwa jijini Dallas tarehe 6 Mei 2024 ili kuendelea kukuza na kuchochea uhusiano wa kibiashara baina ya Tanzania na Marekani.
Uzinduzi huo umehudhuriwa na Viongozi mbalimbali, wafanyabiashara na Wajumbe wa Bodi ya Chemba hiyo ya Biashara wakiongozwa na Mwenyekiti wao Mhe. Kjell Bergh ambaye amewahi kuwa amidi wa Wawakilishi wa Heshima wa Tanzania nchini Marekani.