Mhe. Balozi Dkt. Elsie Sia Kanza ameshiriki kama mwanajopo kwenye Jukwaa la Afrika (Africa Forum) lililoandaliwa na taasisi ya utafiti (think tank) ya Carnegie Endowment for International Peace ya hapa Marekani. Mhe. Balozi alishiriki kwenye mada iliyohusu utekelezaji wa diplomasia nchini Marekani kwa Balozi za nchi za Afrika nchini hapa.