Mhe. Balozi Dkt. Elsie Sia Kanza ameshiriki katika Mkutano wa Maafisa Waandamizi na Wataalamu kutoka nchi zinazonufaika na Programu ya AGOA uliofanyika katika Ofisi za Uwakikishi wa Umoja wa Afrika nchini Marekani hapa Washington, D.C. Mhe. Balozi Kanza pia aliongoza mmoja wa mijadala kwenye Mkutano huo. Mkutano husika ni sehemu ya maandalizi ya Jukwaa la AGOA (AGOA Forum) litakalohusisha Mawaziri wa Biashara kutoka nchi zinazonufaika na AGOA na Marekani. Jukwaa hilo linafanyika hapa Washington, D.C., tarehe 25 na 26 Julai 2024. Kwa mwaka huu Jukwaa la AGOA litajikita kujadili na kuweka msisitizo katika umuhimu wa kuongeza ukomo wa muda wa kutekeleza programu ya AGOA na kuboresha programu hiyo kwa manufaa nchi za Afrika na Marekani.