Mheshimiwa Balozi Dkt. Elsie Sia Kanza alikuwa mgeni rasmi kwenye hafla iliyoandaliwa na International Club of Annapolis (ICA) iliyofanyika katika jiji la Annapolis, jimbo la Maryland. ICA inaundwa na wanachama kutoka kada na sekta mbalimbali. Mhe. Balozi alitumia hafla hiyo kuelelezea vipambele na mikakati ya Serikali katika kudumisha uhusiano wa Kidiplomasia na Kibiashara baina ya Tanzania na Marekani. Kadhalika, aliwakaribisha kuitembelea Tanzania ili kujionea fursa zilizopo katika sekta za kipaumbele na kutembelea vivutio vya utalii.