Mheshimiwa Dkt. Elsie Sia Kanza, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani amekutana na kufanya mazungumzo na Mhe. Bruce Westerman, Mwakilishi kutoka Jimbo la Arkansas ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge la Marekani ya masuala ya Maliasili. Walijadili juhudi za uhifadhi za Tanzania na namna sera za Marekani za masuala ya maliasili na wanyamapori zinavyoweza kusaidia katika kuinua sekta hiyo nchini Tanzania.