Katika mwendelezo wa matukio ya kuadhimisha miaka 60 ya Uhuru wa Tanzania Bara na miaka 60 ya uhusiano kati ya Tanzania na Marekani, tarehe 07 Desemba, 2021, Ubalozi wa Tanzania, Washington, D.C. umefanya Mkutano wa biashara ya bidhaa za kilimo kati ya Tanzania na Marekani. Mkutano huo uliolenga kuimarisha mauzo ya bidhaa za kilimo za Tanzania nchini Marekani, ulishirikisha wafanyabiashara na wadau wa kilimo kutoka Tanzania na Marekani. Mhe. Prof. Adolf Mkenda (Mb.), Waziri wa Kilimo alishiriki pia kwenye Mkutano huo. Meya wa Jiji la Helena West Helena Arkansas Kevin Smith alishiriki mkutano huo