Ubalozi umewapokea wanafunzi kutoka Shule ya Sekondari ya Randolph iliyopo  jiji la Huntsville, Alabama. Wanafunzi hao walikuja kujifunza kuhusu Tanzania ikiwemo historia yetu, utamaduni wetu, vivutio vyetu vya utalii, uchumi wetu na diplomasia yetu, ikiwa ni pamoja na uhusiano na ushirikiano wetu na nchi ya Marekani. Wanafunzi hao waliambatana na walimu wao.