Ubalozi ulifurahi kuwakaribisha Tanzania House washiriki wa programu ya YALI inayodhaminiwa na Serikali ya Marekani. Washiriki hao wamemaliza mafunzo kwenye vyuo mbalimbali hapa Marekani na walikaribishwa Ubalozini kubadilishana mawazo kuhusu masuala waliyojifunza, shughuli za Ubalozini na namna tunavyoweza kushirikiana kwa manufaa ya Taifa. Ubalozi unawatakia vijana hawa kila la heri wanaporejea nyumbani. Aidha, Ubalozi unaishukuru Serikali ya Marekani kwa kutoa mafunzo hayo muhimu kwa vijana wa Kitanzania.