Ubalozi umeungana na nchi nyingine wanachama wa Umoja wa Afrika (AU) kuadhimisha Siku ya Afrika kwa mwaka 2024. Maadhimisho hayo yamefanyika kwenye Uwakilishi wa Umoja wa Afrika hapa Washington, D.C. na kuhudhuriwa na Balozi ambazo ni nchi wanachama wa Umoja wa Afrika, Wawakilishi wa Serikali ya Marekani, wana diaspora wa Afrika, wanazuoni, taasisi na wadau wengine muhimu. Kwa hapa Washington, D.C., maadhimisho hayo yamefanyika tarehe 29 Mei 2024.