Balozi wa Tanzania Nchini Marekani na Mexico, amekutana na kufanya mazungumzo na Watanzania katika Jiji la Houston, Texas nchini Marekani.  Mhe. Balozi alitumia mkutano huo kujitambulisha rasmi katika Jumuiya hiyo na kujadiliana nao masuala mbalimbali muhimu kwa ujenzi wa Taifa. Aidha, Mhe. Balozi alipokea changamoto mbalimbali zinazowakabili Diaspora hao na kuahidi kuzishughulikia, aliahidi pia Ubalozi kuendelea kufanya nao kazi kwa ukaribu.