Mheshimiwa Balozi Dkt. Elsie Sia Kanza alishiriki katika tukio la kuadhimisha St. Patrick’s Day lililoandaliwa na taasisi ya Tanzanian Children’s Project (TCP) kwa lengo la kuchangisha fedha kwa ajili ya miradi ya maendeleo ya jamii nchini Tanzania.  

TCP ni taasisi iliyoanzishwa mwaka 2009 na Knights of Columbus Columbia Council 7559 ambayo imekuwa ikisaidia miradi ya kijamii nchini Tanzania katika sekta za elimu, afya na maji.  

Kwa sasa TCP inajenga shule ya sekondari ya Kikatoliki katika Jimbo la Kahama, Kijiji cha Mahanga (Ushetu, Shinyanga). Pia imekuwa ikisaidia kuboresha miundombinu ya usafi ikiwemo vyoo vya shule.

Katika Hotuba yake, Mhe. Dkt. Balozi Kanza, pamoja na masuala mengine, aliwashukuru TCP kwa shughuli zao ambazo zinaunga mkono juhudi za Serikali katika kuboresha maisha ya wananchi hususan wa kaya za maskini. Pia alisisitiza kuhusu ahadi ya Serikali ya kuendelea kufanya kazi kwa karibu na taasisi za kidini kwa maendeleo ya jamii na umoja wa Kitaifa.