Mhe. Balozi Dkt. Elsie Sia Kanza alipata heshima ya kushiriki kwenye halfa ya chakula cha asubuhi iliyoandaliwa na uongozi wa Ofisi ya Masuala ya Afrika ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani iliyofanyika Wizarani hapo.

Akiwa kwenye hafla hiyo, Mhe. Balozi alipata fursa ya kuzungumza na Bw. Nicholas G. Checker, Kiongozi Mkuu wa Ofisi hiyo, pamoja na viongozi wengine wa Serikali ya Marekani wanaohusika na masuala ya Afrika.

Mazungumzo baina ya Mhe. Balozi na Viongozi hao yalijikita katika masuala yanayolenga kuimarisha uhusiano baina ya Tanzania na Marekani ambao umedumu kwa zaidi ya miongo sita.