Mheshimiwa Balozi Dkt. Elsie Sia Kanza amemwakilisha Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye shughuli ya kusheherekea maisha na mazishi ya Hayati Mchungaji Jesse L. Jackson, Sr., Kiongozi na Mwanaharakati Mashuhuri wa Haki za Kiraia, yaliyofanyika jijini Chicago, Illinois.
Hayati Mchungaji Jackson alikuwa ni rafiki mkubwa wa Tanzania na amewahi kutembelea Tanzania mara kadhaa. Familia ya Hayati Mchungaji Jackson inauendeleza urafiki huo ambao ni wa thamani sana.
Bwana alitoa na Bwana ametwaa, Jina lake Lihimidiwe. Amina.



