Mhe. Balozi Dkt. Elsie Sia Kanza alishiriki sherehe ya sikukuu ya Eid al-Fitr iliyoandaliwa na Jumuiya ya Waislamu Watanzania (TAMCO) wanaoishi kwenye eneo la Washington, D.C., na miji ya pembezoni (DMV). Mhe. Balozi aliwapongeza wanachama wa TAMCO kwa kumaliza salama mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani na kuwatakia sikukuu njema ya Eid al-Fitr.
Aidha, Mhe. Balozi alitoa wito kwa wanadiaspora kuendelea kushikamana na kushirikiana kwa maslahi ya Taifa bila kujali tofauti zao za kiimani na kiitikadi. Pia, aliwaomba kuendelea kuiombea Tanzania na viongozi wa Tanzania wakiongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Ubalozi unawatakia wote heri na baraka tele za Eid al-Fitr!



