Mhe. Balozi Dkt. Elsie Sia Kanza alikuwa ni miongoni mwa wazungumzaji wakuu kwenye Mkutano Mkuu wa 83 wa nchi wanachama wa shirika la International Cotton Advisory Committee (ICAC) lenye makao makuu hapa Washington, D.C. Mkutano huo uliofanyika jijini Bremen, Ujerumani kuanzia tarehe 23 hadi 24 Machi 2026, uliwezesha wadau wakuu wa sekta ya pamba na nguo kujadili fursa zilizopo na kuweka mikakati ya kuvutia uwekezaji kwenye sekta hiyo.
Sekta ya nguo inaendelea kukua kwa kasi duniani ikiwa na mchango wa wastani wa Dola za Marekani trilioni 1.8 kwenye uchumi wa dunia kwa mwaka pamoja na kutoa ajira nyingi ikiwemo kwa wanawake na vijana. Kwa upande wa Tanzania, sekta hii inachangia zaidi ya 95% ya thamani ya mauzo yote ya nchi yetu yanayonufaika na mpango wa AGOA hapa Marekani na kuna fursa kubwa zaidi kwa Tanzania kuendelea kunufaika na soko hilo.
Mkutano huo ulihudhuriwa na viongozi na maafisa waandamizi kutoka Wizara na taasisi mbalimbali za Serikali, sekta binafsi kutoka nchi wanachama wa ICAC ikiwemo vyama vya wafanyabiashara na taasisi za elimu ya juu.



