Mhe. Balozi Dkt. Elsie S. Kanza alifurahi kujumuika na Mhe. Muriel Bowser, Meya wa jiji la Washington, D.C., Viongozi wengine waandamizi wa jiji hilo, pamoja na Mabalozi na wawakilishi wao katika hafla iliyoandaliwa na Meya huyo kwa ajili ya Mabalozi wa nchi mbalimbali zenye uwakilishi hapa Marekani.
Mhe. Balozi alifanya mazungumzo na Meya Bowser kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu kuimarisha uhusiano baina ya Tanzania na Mji huo mkuu wa taifa la Marekani. Pia, alipata fursa ya kuzungumza na Mabalozi na washiriki wengine wa hafla hiyo kwa lengo la kukuza uhusiano baina ya Tanzania na nchi wanazoziwakilisha.
Pamoja na kuwa ni jiji mwenyeji la Ubalozi, Washington, D.C., na miji ya pembezoni mwake (Washington Metropolitan Area) pia ni nyumbani kwa wanadiaspora wengi wa Tanzania.


