Mhe. Balozi Dkt. Elsie S. Kanza amekutana kwa mazungumzo na Viongozi wa taasisi ya hisani ya Convoy of Hope ya hapa Marekani, Bw. Kevin Rose na Bw. Mark Powers.
Kwenye mazungumzo hayo, Viongozi hao walijadili mikakati ya kupanua na kudumisha huduma zinazotolewa na taasisi hiyo nchini Tanzania kupitia progamu za kilimo, utoaji chakula mashuleni na uwezeshaji wanawake kiuchumi.
Convoy of Hope ni taasisi ya kimataifa ya kidini iliyoanzishwa mwaka 1994 hapa Marekani kwa ajili ya kusaidia jamii zenye uhitaji kutatua changamoto mbalimbali ikiwemo umasikini.

