Mhe. Balozi Dkt. Elsie Sia Kanza alishiriki kwenye hafla iliyoandaliwa kwa heshima ya Mabalozi Wanawake, na Seneta Jeanne Shaheen, Kiongozi wa Upinzani wa Kamati ya Mambo ya Nje wa Bunge la Seneti la Marekani pamoja na Seneta Susan Collins, Mwenyekiti wa Kamati ya Masuala ya Bajeti ya Bunge hilo.

Hafla hiyo ilitoa nafasi kwa Mhe. Balozi kukutana na Wabunge mbalimbali wa Bunge la Marekani na Mabalozi kutoka nchi tofauti na kujadili masuala muhimu  katika kuimarisha uhusiano baina ya Tanzania na Marekani na nchi nyingine ambazo Mabalozi wake walishiriki kwenye hafla husika.