Mhe. Balozi Dkt. Elsie Sia Kanza alikuwa mmoja wa wanajopo kwenye mkutano wa masuala ya madini uitwao SAFE Summit uliofanyika Washington, D.C. Mkutano huo ulijadili kukuza na kuchochea uwekezaji kwenye madini adimu (critical minerals) katika nchi zinazoendelea. Tanzania ni miongoni mwa nchi zenye aina mbalimbali ya madini adimu ambayo yanahitajika kwenye maendeleo ya teknolojia na nishati safi. Mhe. Balozi aliwakaribisha wawekezaji kuwekeza nchini Tanzania kwenye sekta ya madini na kutoa wito kwa taasisi ya fedha kurahisisha utoaji wa mitaji kwa wawekezaji.