Tarehe 18 Novemba 2025, Mhe. Balozi Dkt. Elsie Sia Kanza alikutana kwa mazungumzo na viongozi waandamizi wa taasisi ya Rob Walton na  taasisi ya Kimataifa ya masuala ya uhifadhi ( ICCF). Madhumuni ya mkutano huo yalikuwa ni kwa viongozi hao kuarifu kuhusu mipango ya uhifadhi ambayo taasisi zao zimepanga kutekeleza nchini Tanzania. Ikumbukwe kwamba, taasisi hizo zimekuwa vinara wa masuala ya uhifadhi na kushawishi utalii endelevu nchini kwa muda mrefu.

Katika mazungumzo hayo, pamoja na masuala mengine, Mhe. Balozi aliikaribisha mipango ya taasisi hizo ya kupanua wigo wa shughuli zao nchini Tanzania kwani itasaidia juhudi za serikali katika kuboresha shughuli za uhifadhi na utalii.