Mhe. Balozi Dkt. Elsie Sia Kanza amekutana kwa mazungumzo na Bi. Anita Rich, Mwanzilishi na Rais wa taasisi inayojishughulisha na masuala ya uuguzi iitwayo Nurses Heart to Heart ( NHTH) ya hapa Marekani. Wawili hao walijadili mikakati ambayo itawezesha wauguzi wa Tanzania kupata ajira na mafunzo ya uuguzi nchini Marekani. Vilevile, walijadili kuhusu misheni ya wauguzi itakayoongozwa na Bi. Rich kwenda Tanzania mwaka 2026 kwa ajili ya kutoa mafunzo na kuwajengea uwezo wauguzi wa Tanzania. Misheni hiyo pia itaweka kambi ya uchunguzi wa magonjwa mbalimbali kwa kushirikiana na taasisi za Tanzania.
