Mhe. Balozi Dkt. Elsie Sia Kanza ameshiriki na kuzungumza kwenye mkutano wa kujadili uhusiano wa Majiji Dada (sister cities) kati  ya Tanzania na Marekani ulioandaliwa na Taasisi ya Sister Cities International Africa (SCI) ya hapa Marekani. Mkutano huo uliwakutanisha wadau mbalimbali wa majiji dada wakiwemo viongozi wa majiji ya Marekani yenye urafiki na majiji na miji ya Tanzania, viongozi wa SCI, na baadhi ya wawakilishi wa miji dada ya Tanzania. Mhe. Balozi aliwasihi wadau kushirikiana kuongeza idadi ya majiji dada baina ya Tanzania na Marekani na kuimarisha uhusiano baina ya majiji dada yaliyopo kutokana na faida zake kiuchumi, kibiashara, kijamii na kitamaduni. Miji na Majiji 9 ya Tanzania ina uhusiano wa majiji dada na miji ya Marekani.