Mheshimiwa Balozi Dkt. Elsie Sia Kanza amekutana kwa mazungumzo na Mhe. Richard Neal (MA-01), Kiongozi wa Upinzani (Ranking Member) katika Kamati ya Bunge la Wawakilishi la Marekani inayoshughulikia Mapato (The U.S. House Ways and Means Committee).  Kamati hiyo ndiyo inayohusika na masuala ya programu ya AGOA ikiwemo mchakato unaoendelea wa kuongeza muda wa Programu hiyo kabla ya kufikia ukomo mwezi Septemba, 2025. Viongozi hao walijadili fursa za kudumisha uhusiano wa kibiashara na kiuchumi baina ya Marekani na Tanzania ikiwemo mustakabali wa programu ya AGOA.