Katika maadhimisho ya miaka sitini ya Uhuru wa Tanzania Bara na maadhimisho ya miaka sitini ya mahusiano kati ya Tanzania na Marekani, Ubalozi wa Tanzania Nchini Marekani na Mexico umekutana na wadau mbalimbali katika sekta ya biashara, utalii na uwekezaji. Lengo mahususi la mkutano huo ni kutangaza fursa mbalimbali za biashara, utalii na uwekezaji zinazopatikana Nchini Tanzania. Wadau mbalimbali katika sekta za kiuchumi walishiriki. Mkutano huo ulifanyika katika Jiji la Dallas, Texas nchini Marekani.
Ubalozi wa Tanzania Nchini Marekani wakutana na wadau mbalimbali katika sekta za Biashara, Utalii na Uwekezaji.
Balozi Kanza akiwa katika picha ya pamoja na wadau mbalimbali katika sekta za Biashara, Utalii na Uwekezaji.





