Mhe. Balozi alifurahi kukutana na Bw. Frank W. Garcia, Jr., Waziri Msaidizi wa Mambo ya Nje wa Marekani anayeshughulikia Masuala ya Afrika wakati wa hafla iliyoandaliwa na Bw. Garcia kwa ajili ya Mabalozi wa Nchi za Afrika. Wakizungumza wakati wa hafla hiyo, Viongozi hao walikubaliana kuendelea kuchukua hatua mbalimbali kuimarisha uhusiano na ushirikiano baina ya Tanzania na Marekani kwa manufaa ya pande zote.

