Mhe. Balozi Dkt. Elsie Sia Kanza, katika nafasi yake ya Amidi wa Mabalozi wa nchi za SADC jijini Washington, D.C., alikuwa mwenyeji wa Mabalozi na Kaimu Mabalozi kutoka nchi tajwa katika hafla ya kumuaga Mhe. Jaji Esme Jynet Chombo, Balozi wa Jamhuri ya Malawi nchini Marekani aliyemaliza muda wake. Hafla hiyo fupi ilitoa pia fursa kwa Mabalozi hao kujadili masuala mbalimbali yanayowahusu katika kutekeleza majukumu yao hapa Marekani na kuimarisha uhusiano na ushirikiano baina yao.


