Mhe. Balozi Dkt. Elsie Sia Kanza alijumuika na Mabalozi wenzake, Jumuiya ya Kidiplomasia, Viongozi na watumishi wa serikali na Bunge la Marekani, wanadiaspora wa nchi za Afrika, marafiki wa Afrika na wadau mbalimbali katika kusheherekea Siku ya Afrika jijini Washington, D.C.

Pamoja na kufanya mazungumzo na washiriki wengine wa hafla hiyo, Mhe. Balozi alipata pia fursa ya kuzungumza na Bw. Frank W. Garcia, Jr., Waziri Msaidizi wa Mambo ya Nje wa Marekani anayeshughulikia Masuala ya Afrika. Mazungumzo hayo yalijikita katika kuimarisha uhusiano na ushirikiano baina ya Tanzania na nchi hiyo.