Mhe. Balozi Dkt. Elsie S. Kanza alikutana kwa mazungumzo na Bw. David Reinecke kutoka Ofisi ya Masuala ya Anga za Juu ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani pamoja na Bi. Kim Hurst kutoka Shirika la Masuala ya Anga za Juu la Marekani (NASA), na ujumbe wao. Kikao hicho kilijikita kujadili namna Tanzania na Marekani zinavyoweza kuimarisha ushirikiano katika masuala hayo, kwa manufaa ya nchi zote mbili.