Mhe. Balozi Dkt. Elsie S. Kanza alifanya ziara ya kikazi katika Jimbo la Arizona kufuatia mwaliko wa Mhe. Tony Rivero, Mwenyekiti wa Kamati ya Biashara ya Kimataifa ya Bunge la Jimbo la Arizona. Agosti, 2026.
Katika ziara hiyo, Mhe. Balozi alifanya mazungumzo na viongozi wa Arizona Commerce Authority (ACA), Greater Phoenix Economic Council (GPEC), Arizona State University (ASU), pamoja na Mhe. Michael Carbone, Kiongozi wa Wengi (Majority Leader) katika Bunge la Jimbo la Arizona. Mazungumzo hayo yalijikita katika kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Jimbo la Arizona, hususan katika sekta za biashara na uwekezaji, elimu, teknolojia, madini muhimu, afya na maendeleo ya ajira.
Kadhalika, Mhe. Balozi alishiriki katika mkutano na Phoenix Committee on Foreign Relations (PCFR), ambapo aliwasilisha fursa za biashara na uwekezaji zinazopatikana nchini Tanzania.
Kwa ujumla, ziara hiyo imeleta chachu ya kuimarisha uhusiano kati ya Tanzania na Jimbo la Arizona, kufungua fursa mpya za ushirikiano wa kiuchumi na uwekezaji, na kuendeleza diplomasia ya uchumi kwa manufaa ya pande zote mbili.



