Mhe. Balozi Dkt. Elsie Sia Kanza alikuwa ni miongoni mwa wazungumzaji wakuu pamoja na Balozi Jessica Ba kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani, kwenye mkutano wa wafanyabiashara wanawake diaspora wa Kiafrika pamoja na wanawake wa Kimarekani wenye asili ya Afrika ulioandaliwa na taasisi ya ODUNDE jijini Philadelphia. Kwenye mkutano huo, pamoja na masuala mengine, Mhe. Balozi alieleza kuhusu jitihada thabiti zinazoendelea kuchukuliwa na Serikali katika kuboresha mazingira ya biashara nchini Tanzania, mchango wa Tanzania katika kukuza umajumui wa Afrika, fursa za biashara na uwekezaji zinazopatikana nchini Tanzania na aliwakaribisha wafanyabiashara hao kuzichangamkia.
Baadhi ya washiriki hao wameonesha nia ya kutembelea Tanzania ili kujionea fursa hizo.



