Mhe. Dkt. Elsie S. Kanza, Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico alifurahi kumpokea Tanzania House, Mhe. Roelf Meyer, Balozi mpya wa Afrika Kusini nchini Marekani. Mhe. Balozi Meyer alimtembelea Mhe. Balozi Kanza ambaye pia ni Amidi wa Mabalozi wa nchi za SADC, ili kujitambulisha rasmi na kubadilishana mawazo na uzoefu kuhusu masuala mbalimbali yenye maslahi kwa nchi hizo.