Ubalozi uliambatana na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Zanzibar (ZAA) kupokea tuzo iliyotolewa kwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume ambao umeshinda tuzo ya kutoa huduma bora kwa wateja kwenye kipengele cha viwanja vinavyohudumia abiria chini ya milioni 2 kwa mwaka. Tuzo hizo zimetolewa jijini Atlanta, Georgia na taasisi ya Airport Council International (ACI).