Ubalozi ulifurahi kuwakaribisha zaidi ya watu 1,550 waliotembelea Tanzania House tarehe 03 Mei 2025 kupitia programu iitwayo Around the World Embassy Tour: Passport DC. Wageni hao walipata nafasi ya kujionea na kujifunza kuhusu utamaduni, desturi, utalii, historia na fursa mbalimbali zinazopatikana Tanzania.



