Mhe. Balozi Dkt. Elsie Sia Kanza ameshiriki kwenye sherehe za maadhimisho ya miaka 249 ya uhuru wa Marekani iliyoitishwa na Mhe. Marco Rubio, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani. Akiwa kwenye sherehe hizo, pamoja na masuala mengine, Mhe. Balozi alipata pia fursa ya kuzungumza na Mhe. Waziri Rubio na Mhe. Troy Fitrell, Kaimu Naibu Waziri Mdogo wa Mambo ya Nje wa Marekani.


