Mhe. Balozi Dkt. Elsie Sia Kanza ameshiriki kwenye maadhimisho ya Siku ya Afrika yaliyoandaliwa na taasisi ya ONE ya hapa Marekani. Maadhimisho hayo yaliyofanyika ndani ya Bunge la Marekani (Capitol Building), yamehudhuriwa na Viongozi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani, Mabalozi, Wabunge wa Bunge la Wawakilishi la Marekani, taasisi zisizo za Kiserikali na wadau wengine wenye mapenzi na Afrika.