Mhe. Balozi alishiriki kama mgeni maalum kwenye mkutano uliojadili kuhusu umuhimu wa teknolojia ya akili mnemba barani Afrika ambao uliandaliwa na Kituo cha Biashara cha Marekani na Afrika kilicho chini ya Chemba ya Biashara ya Marekani.
Akichangia kwenye mkutano huo, Mhe. Balozi alieleza kuhusu uwepo wa miundombinu wezeshi ya TEHAMA na akili mnemba nchini Tanzania, jitihada zinazofanywa na Serikali kukuza vipaji na kuwaunga mkono wanaojishughulisha na sekta ya TEHAMA na alikaribisha wadau wa sekta hiyo kuwekeza kwenye maeneo yanayohitaji ushirikiano na ubia nchini Tanzania ambayo aliyaainisha.
Pamoja na Mabalozi wa nchi za Afrika na wawakikishi wao, Mkutano huo ulishirikisha pia wawakilishi wa Serikali ya Marekani, viongozi wa kampuni za biashara, wataalamu wa sera za TEHAMA na taasisi za tafiti.



