Katika kuadhimisha Siku ya Kiswahili Duniani mwaka huu, Ubalozi ulishirikiana na Diaspora wa Tanzania na washirika wake wengine kufanya matukio mbalimbali yaliyolenga kutangaza Lugha hiyo adhimu na utamaduni wake mzuri. Tulishirikiana na Jumuiya ya Watanzania wanaoishi Majimbo ya Midwest ya Marekani (Tanzanian Community Association – Midwest USA) ambapo maadhimisho yalifanyika jijini Chicago, Illinois na tuliadhimisha siku hiyo pia na diaspora wa Tanzania wanaoishi jijini Hartford, Connecticut. Kadhalika, tulishirikiana na taasisi za Things To Do DC na  Events DC kutangaza utamaduni wa Kiswahili ikiwemo chakula cha Kiswahili.