Mheshimiwa Balozi Dkt. Elsie Sia Kanza alikutana kwa mazungumzo na Bi. Maria A. Velez, Makamu wa Rais wa kampuni ya SBA ya hapa Marekani anayeshughulikia masuala ya uhusiano na Bw. Ravi Suchak, Mkuu wa Mambo ya Nje, Uendelevu na Sera za Umma wa kampuni ya Helios Towers ya Uingereza ambayo inajihusisha na ujenzi wa miundombinu ya mawasiliano.

Kwenye mazungumzo hayo, viongozi hao walieleza nia ya kampuni zao ya kuongeza uwekezaji kwenye miundombinu ya mawasiliano ili kuendelea kuunga mkono jitihada  za Serikali za kujenga Uchumi wa kidijitaji. Waliarifu kuwa kampuni ya SBA imewekeza nchini Tanzania tangu mwaka 2021 kupitia kampuni tanzu ya MINARA na kampuni ya Hilios Towers imewekeza nchini Tanzania tangu mwaka 2011, ambapo kampuni hizo kwa pamoja zimewekeza kwenye zaidi ya minara ya mawasiliano 6,100.

Viongozi hao pia walitoa shukran kwa Mamlaka mbalimbali za Serikali kutokana na ushirikiano wanaoupata katika kuratibu na kusimamia shughuli za ujenzi na uendeshaji wa miundombinu ya mawasiliano.