Mwezi Mei 2025, Mhe. Balozi Dkt. Elsie Sia Kanza aliungana na ujumbe kutoka Mkoa wa Dar es Salaam ulioongozwa na Dkt. Toba Nguvila, Katibu Tawala wa Mkoa huo ambao ulifanya ziara jijini Dallas, Texas. Madhumuni ya ziara hiyo iliyokuwa ya mafanikio makubwa yalikuwa ni kujifunza kuhusu uendeshaji wa kisasa wa majiji makubwa ikiwa ni sehemu ya mpango mkakati wa Jiji la Dar es Salaam wa kuwa jiji kubwa zaidi (metropolitan city). Pamoja na kukutana na watendaji na taasisi mbalimbali jijini Dallas, Ujumbe huo ulikutana pia kwa mazungumzo na Mhe. Eric Johnson, Meya wa Jiji hilo. Aidha, majiji ya Dar es Salaam na Dallas yapo kwenye hatua za mwisho za kuanzisha uhusiano wa miji dada (sister cities).