Mheshimiwa Elsia Kanza, Balozi wa Tanzania Nchini Marekani na Mexico, amekutana na kufanya mazungumzo na na Meya wa Jiji la Dallas Mheshimiwa Eric Johnson. Katika mazungumzo hayo mambo mbalimbali yalijadiliwa ikiwa ni pamoja na njia zitakazotumika katika kukuza mahusiano ya biashara, utalii na mabadilishano ya kitamaduni kati ya  Dallas naTanzania. Mkutano huo ulifanyika katika ofisi za Jiji hilo zilizopo Dallas, Texas nchini Marekani.

  • Balozi Kanza akibadilishana mawazo na Meya wa Dallas Mhe. Erick Johnson.