Mhe. Balozi Dkt. Elsie Sia Kanza amefurahi kukutana kwa mazungumzo na Mhe. David Douglas Hamadziripi, Balozi Mpya wa Zimbabwe nchini Marekani. Madhumuni ya mazungumzo hayo yalikuwa ni kufahamiana, kujadili masuala yanayohusu ushirikiano wa kihistoria na kidugu kati ya Tanzania na Zimbabwe na kujadili masuala mengine yanayohusu uhusiano baina ya nchi za Afrika na Marekani.
